Nafasi Ya Matangazo

January 11, 2013

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Philipo Mulugo ametangaza  matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili mwaka 2012, ambapo  kiwango cha ufaulu kimepanda kutoka asilimia 45.40 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 64.55 mwaka 2012.



Matokeo hayo yametangazwa  mbele ya  waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam ambapo idadi ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 430,327, kati yao wasichana walikuwa 205,476 na wavulana 224,851, ikiwa  ni upungufu wa watahiniwa 36,240 ikilinganishwa na mwaka 2011 ambao walikuwa 466,567.



“Watahiniwa 386,271 sawa na asilimia 89.76 ya waliosajiliwa, walifanya mtihani wakiwemo wasichana 187,244 na wavulana 199,027, watahiniwa 44,056 sawa na asilimia 10.24 hawakufanya mtihani, kati yao wasichana ni 18,231 na wavulana 25,825” amesema Mulugo.



Aidha Waziri Mulugo amefafanua kuwa watahiniwa 136,946 ambao wameshindwa kupata wastani wa ufaulu wa alama 30 na wale waliofutiwa matokeo yao kutokana na udanganyifu watalazimika kukariri kidato cha pili mwaka 2013.

“Ni vema ikaeleweka kuwa kukariri kidato si adhabu bali ni kutoa fursa nyingine kwa mwanafunzi kuweza kupata maarifa, stadi na ujuzi wa elimu ya sekondari, hivyo ni matumaini yangu kuwa wanafunzi hawa watafanya bidii katika kujifunza na kuzingatia masomo ili waweze kufaulu masomo yao katika kiwango kinachotakiwa” amesisitiza Mulugo.
Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili ulifanyika nchini kote kuanzia tarehe 05 Novemba, 2012 na kumalizika tarehe 16 Novemba, 2012 kukiwa na jumla ya vituo 4,304 vilivyosajili watahiniwa, sawa na ongezeko la vituo 117 ikilinganishwa na ile ya mwaka 2011.
Posted by MROKI On Friday, January 11, 2013 2 comments

2 comments:

  1. good,lakini hujatwambia tunaweza kuyapata website gani hayo matokeo!!!!

    ReplyDelete
  2. Je majina yameshatoka? na kama yametoka tunaomba mtuwekee.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo