Mtaalam wa Astronomia (Astronomy) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Dk. Noorali Jiwaji wa  Kitivo cha Sayansi, Teknologia na Elimu ya Mazingira, akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) wakati wa kuelezea tukio hilo  leo Juni 22.2016, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa chuo hicho kikuu Huria, Profesa Elifas Tozo Bisanda.
Mtaalam wa Astronomia (Astronomy) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Dk. Noorali Jiwaji wa  Kitivo cha Sayansi, Teknologia na Elimu ya Mazingira, akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) wakati wa kuelezea tukio hilo  leo Juni 22.2016, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa chuo hicho kikuu Huria, Profesa Elifas Tozo Bisanda.
 Muonekano endapo mtumiaji atatumia kichujia jua maalum.
Ramani ya Afrika inavyoonekana pindi tukio hilo litalavyokuwa…

Ramani ya Tanzania inavyoonesha itakavyokuwa siku tya tukio.
*************
TUKIO kubwa la angani la kipekee la kupatwa kwa jua usawa wa Tanzania litatokea Septemba 1, 2016, kuanzia saa 4:17 asubuhi hadi Saa 7:56 adhuhuri.

Washabiki na wanataaluma wa anga kutoka duniani kote pamoja na wanasansi, wanafunzi pamoja na jamii ya watanzania wataelekea Rujewa, kusini mwa Tanzania, Karibu na Mkoa wa Mbeya kushuhudia duara la jua linavyobadilika kuwa pete ya jua. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Nchini kote Tanzania mamilioni ya watu watashangaa kuona jua kali la utosi likimegwa kwa zaidi ya asilimia 90 kwa kufunikwa na mwezi katika kupatwa kwa jua lionekane kama hilali nyembamba au kama mwezi mwandamo.

Katika tukio hili la kupatwa kwa jua, watu wanaoishi ndani ya ukanda wenye upana wa kilomita 100 unaokatisha Kusini ya Tanzania kutoka Congo kuelekea Katavi, mbeya, Ruvuma hadi Masasi na kuingia Msumbuji, siku hiyo jua kama duara jembamba kama pete kwa vile asilimia 98 ya jua litakuwa limejificha nyuma ya mwezi.

Kupatwa huko kwa jua kunaweza kuonekana kwa usalama na watazamaji, lakini inabidi kutumia vichuja maalum vya mwanga wa jua.

Tukio la kupatwa ni la kusisimua na la nadra sana kutokea katika maisha ya mtu. Hasa kwa kizazi hiki kipya ambacho kimechangamka kitasisimuliwa sana na tukio la ajabu kama hili na watajifunza Sayansi ili kuelewa kwa nini kinatokea kile wanachokiona.

Kwa hiyo tukio hili linaweza kutumiwa na shule na taasisi za elimu kuendeleza Sayansi na kuvuta wanafunzi kujiendeleza kisayansi na hasa kuelewa mizunguko mbalimbali iliyopo katika mfumo wetu wa sayansi pamoja na anga za juu kwa ujumla. Kuongeza uelewa wa sayansi ni muhimu katika kuelewa maumbile ya ulimwengu wetu.

Kupatwa huku kutatokea siku ya alhamisi ambapo wanafunzi wengi watakuwa mashuleni na ni wakati wa masomo.

Kwavile mchakato wote utaendelea kwa saa nne  hivi , kati ya Saa 4 asubuhi hadi Saa 8 mchana wanafunzi wataweza kushirikiana  kuangalia na kusimulia na kujadili tukio ili kulielewa vizuri na kuandika ripoti madarasani kwao.

Tukio jingine kubwa la kupatwa kwa jua kama hili halitatokea jingine kwa miaka 15 ijayo, kwa hiyo tunahitaji kutumia fursa hili kwa ukamilifu.

Ili kluangalia kupatwa huko, kila mmoja atahitaji kutumia kikinga macho kinachochuja mwanga wa jua kiitwacho kitazamia jua.  Nihatari sana kuangalia jua kwa macho ya moja kwa moja au hata kutumia vichujio vingine vya kiza vilivyotengenezwa kibinafsi.

Kitazamia jua maalum ni kifaa rahisi kilichotengenezwa kutokana na kichuja nguvu ya jua ambacho kinaondoa mionzi haribifu kwa asilimia 99.999. Miwani hiyo maalum ya jua inaweza kutengenezwa Tanzania kwa gharama isiyozidi 500/= kila moja, ikiwemo kuchapa fremu za kadbodi na kichuja nguvu ya jua (polymer filter) kinachoagizwa kutoka Marekani.

Aidha wataalam wanaonya wananchi kutumia tahadhari kwa kutoanaglia tukio hilo moja kwa moja kwa macho yao kwani ni hatari na wanapaswa kutumia miwani maalum ya jua iliyotengenezwa maksusi kwa kazi hiyo.