Nafasi Ya Matangazo

January 17, 2017

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo.

Katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa Fedha 2016/17 yaani kuanzia Julai hadi Disemba 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kodi jumla ya shilingi trilioni 7.27 ikilinganishwa na shilingi trilioni 6.44 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho mwaka wa fedha  2015/16.

Ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2016/17 umeongezeka kwa asilimia 12.74.

Mlinganisho wa makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16 na 2016/17 ni kama ifuatavyo:
MWEZI
MWAKA 2015/16
MWAKA 2016/17
Ongezeko
JULAI
925,384.7
1,069,458.5
15.57
AGOSTI
923,316.9
1,154.222.5
25.01
SEPTEMBA
1,132,310.3
1,378,048.9
21.70
OKTOBA
1,037,179.8
1,131,094.9
9.05
NOVEMBA
1,027, 939.6
1,123,509.7
9.30
DISEMBA
1,403, 189.8
1,414,921.8
0.84
JUMLA
6,449,321.1
7,271,256.26
12.74

Jitihada mbalimbali zinafanywa ili kuhakikisha TRA inaongeza makusanyo kwa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji, kuhimiza maadili mema kwa watumishi, kuboresha mifumo ya ukusanyaji, kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wananchi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato pamoja na kufuatili, kuhimiza matumizi ya mashine za kielektronik na kuhimiza ulipaji wa kodi ya majengo.  

TRA inaendelea kuhimiza wafanyabiashara wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuwasilisha ritani za VAT kabla ya tarehe 20 ya kila mwezi kama ilivyobadilishwa katika Sheria ya Fedha ya 2016.

Pamoja na hayo tunawakumbusha na kuwahimiza wananchi wa Dar es Salaam ambao hawajafanya uhakiki wa taarifa za Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe 31 Januari 2017 ili zoezi hilo liweze kuanzishwa katika mikoa mingine.

TRA inatoa wito kwa wafanyabiashara kulipa kodi stahiki kwa hiari na wakati ili serikali ipate mapato yake ambayo yataiwezesha kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.

Kwa wafanyabiashara wenye madeni ya nyuma wanashauriwa kujitokeza kuonana na Mameneja wa Mikoa na Wilaya kujadiliana jinsi watakavyolipa madeni yao bila kuathiri biashara zao.

Wamiliki wa majengo wanaaswa kutoa ushirikiano kwa kulipia ankara zao za kodi ya majengo kwa hiari .

‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’


Richard M. Kayombo
MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
Posted by MROKI On Tuesday, January 17, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo