Nafasi Ya Matangazo

February 05, 2017


 Marehemu Anorld Swai enzi za Uhai wake
WATU saba wamepoteaza maisha papo hapo katika tukio la ajali ya barabarani iliyotokea leo jioni katika eneo la Mwika mpakani mwa Wilaya ya Rombo na Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro.

Waliopoteza maisha ni pamoja na Mwandishi wa gazeti la Habarileo ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Hai, Anorld Swai.

Akizungumza na Daily News-Habarileo Blog, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,SACP,Wilbroad Mutafungwa alithhibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ajali ilitokea majira ya saa 11 jioni ikihusisha magari mawili na pikipiki maarufu kama Bodaboda.

“Ajali imetokea majira ya saa 11 jioni ambapo watu saba wamepoteza maisha wanne ni kutoka katika Toyota Surf T606 AQZ, mmoja katika bodaboda MC 101 ANC huku wengine wakiwa ni kwenye Fuso T343 BNL,”alisema Kamanda Mutafungwa.

Alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Mwika katika Kijiji cha Mawanjeni katika mpaka wa Wilaya ya Rombo na Wilaya ya Moshi Vijijini na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo inaweza kuwa ni kuharibika kwa mfumo wa Breki wa Fuso iliyokuwa imebena ndizi ikitokea Rombo kwenda Jijini Dar es Salaam.

Mbali na Swai wengio waliopoteza maisha na kutambulika ni Mjumbe wa NEC ya CCM na Katibu wa CWT kutoka Same Ally Mbaga, Mwenyekiti wa UWT Anastazia Malamsha, Edwin Msele, Mwanafunzi  wa mwaka wanne Chuo cha KCMC.

Majeruhi wa ajali hiyo ni Jackson Kimambo - Mwandishi gazeti la Nipashe -  amekimbizwa Hospitali ya KCMC kwa Matibabu pamoja na Mwendesha Bodaboda.

Posted by MROKI On Sunday, February 05, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo