Nafasi Ya Matangazo

May 22, 2017

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahmani Kaniki, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kamati tendaji za shirikisho la wakuu wa Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika, (SARPCCO)  ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika  Mei 24,2017 mkoani Arusha.
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Arusha.
Mkutano mkuu wa  mwaka wa Shirikisho la wakuu wa Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) unatarajia kufanyika jumatano Mei 24, 2017 mkoani Arusha chini ya mwenyekiti wa Shirikisho hilo kwa kipindi hiki ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu. 
Taarifa iliyotoilewa na Msemaji wa Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Advera Bulimba imesema mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na utahudhuruwiwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi kutoka SADC na wale wa Shirikisho la Polisi wa kimataifa INTERPOL ambapo tayari kamati tendaji za shirikisho hilo zinaendelea na mikutano yake kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huo mkuu.
Bulimba alisema katika mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya Operesheni za pamoja katika kubaini na kukabiliana na makosa  mbalimbali yakiwemo  dawa za kulevya, wizi wa magari, usafirishaji haramu wa binadamu na ugaidi.
“Vilevile, mkutano huu utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa Upelelezi wa SARPCCO pamoja na kamati tendaji za sheria, Mafunzo na kamati tendaji ya Jinsia na watoto baada ya mkutano wao uliofanyika mwezi Machi mjini Bagamoyo” Alisema Bulimba.
SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu. Shirikisho hilo linaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, DRC, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Syshelis.
Posted by MROKI On Monday, May 22, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo