Nafasi Ya Matangazo

June 26, 2017

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi Dkt.Kezia, cheti cha ushiriki wa mafunzo ya tathmini ya ajali na majeraha kwa mfanyakazi aliyeumia wakati akitekeleza majukumu yake mahala pa kazi,  wakati wa kilele cha mafunzo ya siku tano kwa madaktari kutoka hospitali za umma na binafsi za jijini Dar es Salaam. Jumla ya madaktari 70 kutoka hospitali 35 walishiriki.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAFUNZO ya siku tano kwa madaktari yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ili kuwajengea uelewa wa namna ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi yamemalizika kwa washiriki kutunukiwwa vyeti.
Mafunzo hayo yaliyofunhga na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba makao makuu ya Mfuko huo, jingo la GEPF barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Juni 23, 2017, yaliwaleta pamoja madaktari 70 kutoka hospitali mbalimbali za umma na binafsi jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yaliyogusa maeneo mbalimbali pia yaliwawezesha madaktari hao kujifunza Muongozo mpya unaohusu namna ya kufanya tahmini kabla ya kumlipa fidia stahiki Mfanyakazi aliepata madhara mahala pa kazi.
Akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo hayo,  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw  Masha Mshomba, alisema kuwa  ni iani ya Mfuko kuwa Madaktari hao wamefaifika na mafunzo hayo na yatawezesha ufanisi katika kjutoa huduma hizo kwa wafanyakazi waliopata magonjwa au kuumia wakati wakiwa kazini.

 Dkt.Benjamin Najimu Mohammed, akizungumz kwa niaba ya madaktari wenzake. "Nia ya mafunzo haya ni kwenda kuwasaidia watanzania wenzetu kwa niaba ya wenzangu napenda kuushukuru Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, kwa kutambua umuhimu wa ushiriki wetu katika mafunzo haya ili hatimaye kuwasaidia walengwa ambao ni watanzania wenetu." Alisema Dkt. Mohammed kutoka hospitali ya Kairuki ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa jopo la wataalamu walioendesha mafunzo hayo, Dkt.Robert Mhina kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt.Arnold Mtenga
  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt.Aida O. Salim
   Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt.Alex Shuli
 Dkt. Machumani Kiwanga akisikilzia kwa makini hotuba ya ufungaji

 Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia),  akifuatilia kwa makini hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo kwa wataalamu hao wa afya.
 Washiriki wakisikiliza hotuba
Bw. Masha Mshomba, (kushoto), Mkurugenzi Mkuu, WCF akiwa na Daktari bingwa wa upasuaji na majeruhi kutoka tasisi ya Mifupa MOI, Dkt. Robert Mhina, ambaye ndiye alijkuwa mwenyekiti wa jopo la wataalamu waliotoa mafunzo hayo
Posted by MROKI On Monday, June 26, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo