Nafasi Ya Matangazo

December 06, 2017

Washiriki wa Mkutano huo wakiendelea na mijadala
Na Mwandishi Wetu
WAZO la kutumia fursa  ya faida ya kuthamini thamani katika sekta ya madini  limeuteka  mkutano wa bara la Afrika unaoendelea nchini Ghana uliojikita kujadili namna ya kuongeza thamani katika sekta ya Uchimbaji.

Wajumbe  wa mkutano huo ambao ulianza jijini Accra, jana wamebainisha kuwa mataifa mengi  ambayo  yana utajiri  mkubwa wa  madini barani Afrika sio tu  yana faidika kwa  kiwango  kidogo kutokana na rasilimali zao kupitia mauzo ya nje ya madini  ghafi  bali  pia faida za  ajira  na suala la  kuwajengea uwezo wa fedha limekuwa kidogo  hivyo kuwafanya wawe wahanga wa kushuka kwa thamani ya masoko ya rasilimali duniani.

Akifungua mkutano huo wa siku mbili, Makamu wa Rais wa Ghana, Dkt.  Mahamudu Bawumia, alisema kuwa Afrika ina asilimia 30 ya rasilimali za madini duniani, asilimia 12 ya hifadhi ya mafuta duniani na asilimia 42 ya hifadhi za dhahabu za dunia lakini bado umaskini unaendelea katika bara hili.

 "Dhana ambayo tumekuwa tukiifanya ama kuiendeleza tangu kujipatia Uhuru inahitaji mabadiliko. Tumekwenda katika njia ya uchimbaji wa rasilimali za asili lakini hakuna faida.Hivyo, mtazamo mpya  na  mabadiliko yatahitaji  kwa  bara hili  katika suala la kuuza nje bidhaa ghafi ," alisema

 Dkt  Bawumia alibainisha kuwa jambo hilo linawezekana kufanikiwa kupitia kuongeza thamani bidhaa zetu tunazouza  nje  badala  ya kuziuza  zikiwa ghafi.

Kwa upande wake,  Mkuu wa Utafiti na Sera katika Taasisi ya Uongozi, Dennis Rweyemamu, alisema Afrika ina wingi wa rasilimali za ziada lakini inakosa utaalamu wa kutengeneza  madini hayo  na kuyafanya  yawe bidhaa zenye  thamani kubwa.

" Madini  mengi yanayochimbwa na  kusafirisha  kuzwa nje  yana kuwa  bado  katika hali ya kuwa ghafi, na  mchakato wa kuyaongezea thamani hufanyiki  kwingineko ,  hivyo kufanya mataifa  ya Kiafrika yenye utajiri wa madini  yapate  faidi kidogo kutokana na  mauzo hayo  ya rasilimali  ghafi  na pia kupunguza ajira  faida za ajira  na kufanya mataifa hayo utegemezi wa masoko ya rasilimali duniani. "Rweyemamu alisema.

Aliwaambia wajumbe kuwa katika nchi nyingi za kiafrika, uchimbaji wa rasilimali ni sekta inayojitenga  kutoka katika shughuli nyingine za kiuchumi, na kuongeza kuwa kimsingi uzalishaji unaotumia mitambo zaidi  umetoa nafasi finyu  kwa nchi mwenyeji katika uzalishaji katika masuala ya ugavi na  ajira .

"Hii inamaanisha kuwa  katika sekta ya uchimbaji ya madini imeshindwa kuwa chanzo cha ukuaji wa uchumi kupitia kutengeneza  ajira, mahitaji ya bidhaa za ndani na huduma pamoja na kutoa ujuzi na teknolojia kwa  nchi husika ."

Pia alibainisha kuwa nchi  zimekuwa zinategemea  kupata mapato kupitia mirahaba,  faida zitokanazo na hisa na makampuni , gawio  kwa serikali uliofanyika usawa kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya  maendeleo.

Aidha alibainisha kuwa kwa sasa kuna ongezeka la ufahamu  hivyo alisema, faida kubwa zaidi na endelevu inaweza kupatikana kutoka kwa kila gramu ya madini yanayochimbwa  kupitia ongezeko la  thamani.
Posted by MROKI On Wednesday, December 06, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo