Nafasi Ya Matangazo

December 04, 2017

Mkuu wa Wilaya Kakonko mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala (kushoto waliosimama) akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama wakiwa wamewashikilia watuhumiwa watano ambao walikutwa na Ng'ombe 93 wakiwa katika Kijiji cha Bukiriro, Kata ya Gwanumpu Tarafa ya Kasanda Wilayani humo wakitokea nchini Burundi.
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
KAMATI ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya kakonko ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo kanali Hosea Ndagala wamekamata Ng'ombe 93 na raia wanne kutoka Nchi ya Burundi walioingizwa Nchini kinyume cha sheria na wachungaji kutoka Nchini humo.

Akizungumza na Waandishi wa habari jana baada ya oparesheni ya kufukuza mifugu kutoka Nje ya Nchi iliyoingizwa kinyume na utaratibu Mkuu huyo alisema Ng'ombe hizo zilikamatwa katika Kijiji cha Bukiriro kata ya Gwanumpu ambapo baadhi ya wananchi wa kijiji hicho walikuwa wamewahifadhi.

Aidha Ndagala aliwataja wanaoshikiliwa na jeshi la polisi ni Ntirampeba gerald, Ndoayo Yusto, Myosaba Joris na Ndebe Lema wote wakiwa ni raia wa Burundi. Ng'ombe hao waliokamatwa walikuwa wamewekeshwa kwa Bw. Gozbati Moses ng'ombe 27 na Bw. Kaitila Mgiligiji ng'ombe 66 wakazi wa kijiji cha Bukiriro, kata ya Gwanumpu Tarafa ya Kasanda Wilayani humo.

"Niwaombe viongozi Wote hususani wa vijiji vya mpakani kuwajibika na kuhakikisha kuwa hakuna mifugo yoyote kutoka nchi jirani inayoingia au kuwekeshwa kwa mtu ye yote atakae kutwa anahifadhi mifugo hiyo atachukuliwa hatua za kisheria msigeuze Nchi yetu kuwa shamba la bibi, zoezi hili ni endelevu", alisema Mkuu huyo.

Aidha, Kanali Ndagala aliwashukuru wananchi waliotoa taarifa kufanikisha zoezi hilo na kuwataka kuendelea kutoa taarifa wanapobaini uwepo wa mifugo kutoka nje ya Nchi na kuwaagiza wananchi Wote wenye tabia ya kuwekeshwa mifugo kutoka Nchi jirani na kuajiri wageni kinyume na taratibu kuacha mara moja.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Gwanumpu Toi Butono alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya Wananchi kihifadhi Wahamiaji haramu pamoja na mifugo yao hali inayoweza kuongeza uhalifu katika kata hiyo kutokana na baadhi ya warundi wanaokaribishwa kujihusisha na vitendo viovu.

Hata hivyo aliwaomba Wananchi kuacha tabia hiyo na kuendelea kuzuia mifugo yao katika Wilaya hiyo ilikuweza kudumisha amani na usalama katika Kata hiyo.
Posted by MROKI On Monday, December 04, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo