Nafasi Ya Matangazo

April 24, 2018


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wa tano kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa Nne kulia) Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson (wa tatu kulia) na baadhi ya Viongozi wakifunua kitambaa kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kemikali cha Msufini (T) Ltd, Mlandizi mkoa wa Pwani, leo. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)

Wakifurahia baada ya kuweka Jiwe la Msingi

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi TPSF, Regnald Mengi, akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kemikali cha Msufini (T) Ltd, Mlandizi mkoa wa Pwani,

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akihutubia kwa niaba ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kemikali cha Msufini (T) Ltd, Mlandizi mkoa wa Pwani
******************************
SERIKALI imezindua mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kemikali za kutengeneza dawa za kusafishia maji kitakachogharimu sh. Bilioni 256.

Uzinduzi huo umefanyika eneo la Mlandizi Msufini mkoani Pwani jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kwa niaba ya Makamu wa Rais, Samiah Suluhu Hassan.

Mwijage alisema mradi huo ukikamilika utasaidia serikali kuokoa kiasi cha fedha kilochokuwa kikitumika kununua dawa hiyo nje za nchi.

" Mradi huo ni wa tatu kwa ukubwa Afrika na kwa sasa tunatarajia kuzindua viwanda vingine tisa vilivyo na viwango. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Na ili kuhakikisha adhma ya viwanda inafanikiwa nitatoa eneo langu kwa ajili kujenga jumba la utamaduni wa viwanda, " alisema.

Mwijage aliwataka Watanzania kujenga uthubutu wa kuwekeza kwenye viwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi.

4Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Justine Lumbert , alimwakikishia Rais Dk.John Magufuli kuwa anacho kikosi mahiri nchini kwa ajili ya jenzi wa viwanda kwa mkoa wa Pwani.

Alisema mradi huo wa dawa ni mkubwa barani Afrika hivyo utaisaidia nchi kutengeneza aina ya dawa ya Chlorine itakakayotumika kusafisha maji.

" Utengenezaji wa dawa hiyo hutumia chumvi, sasa hakuna chumvi yoyote itakayouzwa nje ya nchi hadi mahitaji ya kiwanda hicho yatakapojitosheleza kwa sababu bidhaa zitakazotengenezwa zitakuwa na soko la asilimia 20 ndani ya nchi na 80 nje ya nchi," alisema.

Mkurugenzi huyo ujenzi wa mradi huo utagharimu kiasi cha sh. Bilioni 256 kwa eneo la hekari nane na utakamilika ndani ya miezi 23.

" Tunaiomba serikali kuweka sheria na kanuni stahiki zitakazosaidia kulinda bidhaa na malighafi ya chumvi itakayotumiwa na mradi huu," alisema.

Lumbert alitaja faida za mradi huo, utasaidia kuingizia taifa fedha za kigeni, kuokoa fedha za kununulia dawa nje, kuokoa gharama za matumizi ya kusafisha maji nchini na kuongeza ajira rasmi kwa vijana takribani 700.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe, alimuagiza Mkurugezi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja, ndani ya siku tatu anakutana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo kwa ajili ya ujenzi wa pipa kubwa la maji eneo la Mlandizi ili kuhakikisha yanapatikana eneo hilo kwa urahisi.

" Kwa Wizara yangu itabadilisha muundo wa ununuzi kwani tutakuwa tukinunua ununuzi wa pamoja kuanzia Julai mwaka huu sasa wizara yangu haitakwenda kununua sawa ya kusafisha maji nje wakati itakuwa ikipatikana nchini," alisema.

Kamwele alizitaja aina ya upungufu uliokuwepo katika wizara yake kuwa ni utengenezaji wa mabomba ya chuma cha pua na dawa ya kusafisha maji kwa haraka iliyo na uwezo wa kuzamisha vumbi na matope kwa haraka.

Naye Mhandisi Ndikilo alisema mradi wa kiwanda hicho ni wa tofauti Afrika Mashariki kwa sababu Afrika kinapatikana nchi ya Misri na Nigeria.

" Wawekezaji tambueni ya kuwa mkoa wa Pwani uko salama kwa hiyo msipigiwe kelele na mitandao ya kijamii.

"Kiwanda hicho kinahitaji tani 2500 ya chumvi kwa mwezi kwa hiyo wazalishaji changamkieni fursa hiyo kwa sababu hakuna chumvi itakayochukuluwa nje ya nchi," alisema.


Sehemu ya wageni waalikwa



Wasanii wa Bendi ya JKT wakitoa burudani.....

Baadhi ya wafanyakazi wa Junaco wakisebeneka katika hafla hiyo

Mgeni rasmi akielekea meza kuu

Naibu Spika akielekea Meza Kuu

Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa, akizungumza wakati wa hafla hiyo.



Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya zoezi la uwekaji Jiwe la Msingi. Kushoto ni Naibi Spika wa Bunge la Jamhuri, Tulia Ackson.

Picha za kumbukumbu baadhi ya wageni waalikwa katika jiwe la msingi, Papii Kocha akisoo love na wadau
Picha za kumbukumbu




Picha za kumbukumbu...
Posted by MROKI On Tuesday, April 24, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo