Nafasi Ya Matangazo

September 24, 2016Katika kuhakikisha kero ya kukosa Maji inakwisha kwenye maeneo mbalimbali yanayowazunguka wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) imezindua vizimba maalum vya Majisafi katika mitaa mbalimbali ya kata ya Manzese Mpakani iliyopo wilaya ya Kinondoni ili  kuwapunguzia wakazi wa maeneo hayo adhaa ya kutafuta Majisafi na salama kutoka umbali mrefu.

Akizungumza katika uzinduzi huo wa vizimba vya Majisafi, Meneja wa Dawasco mkoa wa Magomeni Mhandisi Pascal Fumbuka ameleeza kuwa wamejenga jumla ya vizimba saba vya Majisafi ambapo mtaa wa mchafu wamejenga vizimba vitatu na katika mtaa wa Muhltani wamejenga vizimba vinne na vizimba hivyo vya Majisafi vinatarajia kuhudumia wakazi zaidi ya elfu moja wa maeneo hayo.

“Katika kutatua kero ya Maji hapa Manzese mpakani tumejenga vizimba vya Majisafi saba ambapo tunatarajia wakazi zaidi wa elfu moja watanufaika na hivi vizimba vya Majisafi hata hivyo kutokana na ujenzi holela wa makazi ya watu imetuwia ngumu kufikisha bomba kwa kila mkazi ila kwa vizimba vya Majisafi tuamini vitaondoa kabisa kero ya Maji kwani kwa kizimba kimoja tu kina bomba nane na Maji yanapresha kubwa hivyo havitaleta msongamano pamoja usumbufu kwa wakazi pale watakapokuwa wanakinga Maji” alisema Fumbuka.

Kwa upande wa mwenyekiti wa serikali ya mtaa ya Muhltani Bw. Sudy Makamba ameishukuru Dawasco kwa kujenga vizimba hivyo vya Majisafi kwani wakazi wa mtaa wake wamekuwa wakipata adhaa ya kutafuta Majisafi na salama kwa muda mrefu hivyo amewataka wananchi kuvituza pamoja na kulinda miundombinu ya Maji iliyopo katika mtaa wao .

“Nawashukuru sana Dawasco magomeni na uongozi wake kwa kutukumbuka na kujenga vizimba hivi vya Majisafi ambavyo vitasaidia kuondoa kero ya Maji katika mtaa wetu ambao umekuwa haupati Majisafi kwa muda mrefu ila pia natumia fursa hii kuwasihi wakazi wote wa mtaa huu kutuza hivi vizimba pamoja na miundombinu kwani tukiharibu tutarudi katika shida tuliyokuwa nayo mwanzo”  alisema Makamba.

Nae mkazi wa mtaa wa mchafu bi. Martha Faraji amesema kuwa  vizimba hivyo vya Majisafi ni mkombozi mkubwa kwao haswa wanawake ambao wamekuwa wakihangaika na adhaa ya  kukosa majisafi na salama kwa kipindi kirefu ila ameiomba Dawasco kuongeza vizimba hivyo kwenye mtaa wao ilikuepukana na msongamano kwenye vizimba hivyo.

“vizimba hivi vya Majisafi kwa kweli vimetuokoa sisi wanawake wa mtaa wa mchafu maana tulikuwa tunapata shida mno maana tunahangaika kupata majisafi na kwa bei ya juu ambayo sisi watu wakawaida inatuwia ngumu kumudu ila tunaomba Dawasco wajenge vingi ilikusiwe na foleni wakati tunaenda kukinga Maji” alisema Faraji.
Posted by MROKI On Saturday, September 24, 2016 No comments


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wapili kulia) akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe wilayani Kasulu. Kulia ni Mbunge wa Kasulu, Daniel Nsanzugwanko na kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi akizungumza na wananchi wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi. 
*************
WANANCHI wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, wanataraji kuanza kufaidi umeme wa REA pindi awamu ya pili ya mradi huo itakapo kamilika mwishoni mwa  Octoba 2016.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, alipotembelea miundombinu ya Umeme wa REA katika Wilaya ya Kasulu.

Waziri Muhongo yupo katika ziara ya siku tano mkoani Kigoma kuangalia utekelezaji wa awamu ya pili ya miradi ya REA mkoani humo na Wilayani Kasulu aliongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Martin Mkisi.

Prof Muhongo, akiambatana na Wahandisi wa Tanesco, REA na Wakandarasi wanaojenga miundombinu hiyo, wamezungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe na Heru Juu Wilayani Kasulu.

 Aidha katika awamu ya tatu, vijiji vipatavyo 29 vitakamilishiwa huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi, amewataka wananchi kutunza miundombinu ya umeme, kuchangamkia fursa za kufunga umeme wa bei rahisi na kujitokeza kwa wingi kwenye  mafunzo yatakayotolewa na Tanesco kuhusu umeme wa REA.

Pia amewaagiza wakandarasi kukamilisha usambazaji wa huduma hiyo ifikapo Octoba 30 mwaka huu bila kuongeza siku hata moja.
Posted by MROKI On Saturday, September 24, 2016 No comments
 Baadhi ya wafanyakazi katika matembezi ya kujenga afya

 Baadhi ya wafanyakazi katika matembezi ya kujenga afya

Baadhi ya wafanyakazi katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mashindano

Baadhi ya wafanyakazi katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mashindanoBaadhi ya wafanyakazi katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mashindanoBaadhi ya wafanyakazi katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mashindano.
*******
MATEMBEZI ya kujenga afya ya September Fun run yalifanyika jijini Dar es salaam katika maeneo ya Oysterbay chini ya udhamini wa kinywaji cha Grand Malta ambapo yaliwashirikisha wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali pamoja na familia zao ambapo pia walipata fursa ya kufanya mazoezi mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha afya .


Miongoni mwa washiriki wa matembezi haya ya kilometa 10 ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group ambao wamekuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara kupitia programu ya kampuni yao inayojulikana kama Afya Kwanza ambayo inahamasisha ufanyaji wa mazoezi kwa wafanakazi na familia zao ambapo pia wamekuwa wakipimwa afya zao na kupatiwa elimu ya afya na umuhimu wa kupata lishe bora.

Posted by MROKI On Saturday, September 24, 2016 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo